Site icon A24TV News

WAZIRI KIJAJI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WAINDONESIA, KUBORESHA USHIRIKIANO WA BIASHARA

 

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Indonesia na Balozi wa Indonesia nchini Mhe. Tri Yogo Jatmiko Disemba 6, 2022 katika Ofisi za Wizara, jijini Dodoma.

Waziri Kijaji amemhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania iko tayali kuendeleza ushirikiani baina ya nchi hizo na iko tayari kuwezesha miradi ya uwekezaji hususani katika sekta ya kilimo hasa katika uongezaji wa mnyororo wa thamani katika mazao ambayo nchi hiyo imepanga kuyaendeleza kama vile karafuu ili kuongeza ajira na kipato kwa wanzania.