Site icon A24TV News

WAITIMU WAASWA KUJIKITA KATIKA AJIRA NIDHAMU SEHEMU YA KAZI

Na Geofrey Steven,Arusha.

Kaimu afisa elimu sekondari mkoa wa Arusha Emmanuel Mahundo amewataka vijana kuwa waadilifu ,waaminifu pamoja na kuendelea kujiendeleza kimasomo ili kukidhi katika soko la ajira duniani

Ameyasema hayo katika maafali ya 5.katika chuo cha Volcano kilichopo mkoani Arusha na kubainisha kuwa soko la ufundi stadi ni kubwa na ni la dunia nzima hivyo ni vyema wakaendelea kujiendeleza na elimu za mafunzo stadi ili kuweza kufikia ndoto zao.

“Baada ya mfumo rasmi serikali ikaona ni vyema kukawa na elimu ya ufundi kwani serikali imetoa fursa katika elimu hii,”.Alisema Mahundo.

Alisema kama wanafunzi hao wameshindwa katika elimu rasmi serikali imeweka mikakati kabambe ili kupata elimu ya ziada na kuweza kujiajiri.

“Zamani tulikuwa na elimu ya kujitegemea, ndio hii sasa elimu ya vitendo ikiwa ukipata elimu hiyo utanufaika na mambo mbalimbali,”.

Mahundi alisema kupitia elimu hii Muhitimu anauwezo wa kujiajiri,inafanya suluhu ya matatizo kwa haraka, na kujipatia kipato tofauti na elimu ya kawaida.

Huku akiwataka wazazi kuwapeleka watoto wao katika vyuo vya ufundi ili mtoto aweze kupata ujuzi na kujiongezea kipato.

Nae mkuu wa chuo hicho Lazaro Thobias amesema chuo hicho kimefanikiwa kuwaunganisha wanafunzi wanaohitimu kila mwaka kwenye soko la ajira kwa zaidi ya asilimia 90.

Alisema moja ya manufaa katika chuo hiko ni wanafunzi wengi waliohitimu wamefanikiwa kufanya kazi katika mashirika ya serikali na sekta binafsi pamoja na hifadhi mbalimbali ikiwa ni juhudi binafsi za uongozi wa chuo

Katika kila mafaniko hakukosi changamoto,Neema Laizer ni mmoja wa wanafunzi katika chuo cha Volcano anabainisha uhabawa wa vifaa vya kufundishia kwa vitendo hususani katika kozi zinazoendana na ufundi umeme,upungufu wa viti na meza na kupelekea kutoingiza wanafunzi wengi kwa wakati mmoja lakini pia uhaba wa vifaa vya michezo zikiwa kama changamoto zinazowakabili chuoni hapo.

Laizer ameiomba serikali mkoani humo kuzifanyia kazi changamoto hizo ili kuboresha elimu kwa vitendo katika chuo hicho na kupata wataalamu walio bobea katika fani mbalimbali.