Site icon A24TV News

PICHA YA NABII MKUU DKT GEORDAVIE YAPANDISHWA KATIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO.

Na Geofrey Stephen kilimanjaro

Mabalozi wa Nabii Mkuu Dkt GeorDavie  wamesherehekea miaka 61 ya uhuru wa Tanzania kwa kupandisha picha ya Nabii Mkuu Mh Dkt Geordavie kama njia ya kutambua mchango wake katika kuisaidia jamii ya watanzania na Dunia kwa ujumla.

Pia wamepandisha picha ya Nabii Mkuu kama njia mojawapo ya kuitangazia dunia na mataifa mchango wa Nabii Mkuu Dkt Geordavie kwa namna anavyojitoa kuwasaidia watu wasiojiweza.

Umoja huo ambao ni mabalozi wa kazi ambazo amekua akizifanya Nabii Mkuu Dkt Geordavie wamekuwa wakizitangaza katika mitandao ya kijamii walianza rasmi mchakato wa kupandisha picha hiyo mnamo Desemba 5 mwaka huu kuelekea kilele cha mlima Kilimanjaro mnamo tarehe 9 Desemba ambayo ni siku ya uhuru wa Tanzania.

Tanzania na Dunia kwa ujumla ilikuwa ikifuatilia zoezi la viongozi wa serikali pamoja na wananchi zaidi ya 200 waliokuwa wakiupanda mlima huo mkubwa barani Africa.

Katika maadhimisho hayo ya siku ya Uhuru mabalozi hao walisema kwamba kutokana na umuhimu na kutambua kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na Nabii Mkuu Mh Geordavie wameona ni vyema kutambua mchango wake kwa kupandisha picha hiyo mlimani ili kwa kuwa Nabii Mkuu Dkt Geordavie amekua sehemu ya kutatua changamoto za wananchi.

Mabalozi hao wamepandisha kileleni picha ya Nabii Mkuu Dkt Geordavie ili kufikisha ujumbe kwamba ni mtu ambaye pamoja na kwamba ni mtumishi wa Mungu lakini amekuwa sehemu ya kuwainua wasiojiweza na kuwainua kimaisha.

Mabalozi hao wamekua wakivutiwa na kazi za Nabii Mkuu ikiwemo kujitolea kwa kuwapa mitaji wakina mama na vijana ambapo katika siku za hivi karibuni amesaidia makundi mbalimbali mitaji ya biashara ikiwemo bajaji na piki piki bila kujali dini wala kabila.

Nabii Mkuu GeorDavie amekuwa kivutio katika siku za hivi karibuni katika mitandao ya kijamii kutokana na aina yake ya kuguswa na kujitolea kwa watu wenye mahitaji maalumu.

Nabii Mkuu Dkt Geordavie amekuwa akijitolea kusaidia makundi mbalimbali kwa kushirikiana na watumishi wengine wakiwemo wachungaji Maaskofu na Masheikh kujenga makanisa pamoja na misikiti kwa kutambua kwamba Mungu amemtuma kuwafikia mataifa yote

Mabalozi hao wa kazi za Nabii Mkuu Dkt Geordavie wameeleza kwamba watendelea kutangaza kazi zote za Mh Nabii Mkuu kwa kazi zake ambapo hivi karibuni walifika mbele ya madhabau yake ambapo aliwashika mkono katika kufungua kutekeleza majukumu yao mbalimbali ya kuhabarisha umma ndani ya jamii ya Kitanzania.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mabalozi hao wamemwagia sifa Nabii Mkuu Dkt Geordavie kwa namna anavyosaidia jamii bila kujali dini,rangi wala kabila.

Mwisho.