Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»DC NJOMBE:WANAFUNZI KUNUNULIWA GARI NA KUPANGISHIWA NYUMBA NA WANAUME NAO NI UKATILI WA KIJINSIA

    DC NJOMBE:WANAFUNZI KUNUNULIWA GARI NA KUPANGISHIWA NYUMBA NA WANAUME NAO NI UKATILI WA KIJINSIA

    0
    By arushatv on December 6, 2022 Habari

    Na Mwandishi wa A24Tv .

    Wakati Tanzania ikiendelea kupinga ukatili wa Kijinsia kupitia siku 16 za kabilibiana na janga hilo mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema hata vitendo vinavyofanywa kwa wanafunzi mbalimbali ikiwemo kuwanunulia simu,gari na hata kuwapangishia nyumba ni ukatili pia unaopaswa kupigwa vita.

    Katika mdahalo wa kupinga ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na shirika la wanawake katika sheria na maendeleo barani Afrika @wildaftz kupitia mradi wa mwanamke Imara ukihusisha wanafunzo wa vyuo vikuu na vyuo vya kati takribani sita Kasongwa amesema ipo haja ya kuongeza nguvu katika kupinga ukatili huo kwa wanafunzi na watoto nchini.

    Aidha Kasongwa amesema vyombo vya habari vinatakiwa kuendelea kutangaza habari za ukatili kwa nguvu na hatua zinazochukuliwa ili kukomesha vitendo hivyo.

    Hata hivyo ameonesha masikitiko makubwa juu ya kuwapo kwa baadhi ya wanaume wanaojiingiza kwenye mapenzi ya jinsia moja huku akitaka sheria zichukua mkondo wake dhidi ya watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

    Susan Kawanga ni Mratibu wa mradi wa Mwanamke Imara toka shirika la Wildaf ambaye amesema wameandaa mdahalo huo katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ukiwa na lengo la kutaka kujadili changamoto zilizopo vyuoni hususani rushwa za ngono na ukatili mwingine.

    Post Views: 134
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleHABARI KUBWA , SHEREHE ZA UHURU ZAFUTWA MILION 960 KUJENGA MABWENI YA WENYE ULEMAVU ! MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV
    Next Article HABARI KUBWA KATIKA MAGAZETI YA LEO NA A24TV ! PROFESA ASSAD, ANASTAHILI KULIPWA MSHAHARA MPAKA 2026

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.