Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Uncategorized»WAZIRI KIJAJI TUTUMIE LUGHA YA KISWAHILI KUONDOA CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA

    WAZIRI KIJAJI TUTUMIE LUGHA YA KISWAHILI KUONDOA CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA

    0
    By arushatv on November 24, 2022 Uncategorized

    Na Mwandishi wa A24Tv .

    Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amezihamasisha nchi za Afrika kutumia lugha ya kiswahili ili kuondoa changamoto ya lugha katika kufanya biashara ili kuleta maendeleo ya viwanda.

    Aidha Waziri Kijaji amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kuzalisha bidhaa zenye viwango vya kimataifa ili kikidhi usindani wanapotumia fursa za soko la Eneo Huru la Biashara Afrika ( AfCFTA).

    Waziri Kijaji ameyasema hayo Novemba 23, 2022 wakati akishiriki katika Mkutano ngazi ya Baraza la Utendaji la Mawaziri katika Mkutano wa 17 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Maendeleo ya Viwanda Barani Afrika uliofanyika Novemba 20-25, 2022 Niamey, Niger.

    Aidha, Waziri Kijaji atamwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano ngazi ya Wakuu wa Nchi na Serikali unatarajiwa kufanyika tarehe 25 Novemba, 2022.

    Post Views: 203
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMAMA ADAIWA KUUA WATOTO WAKE KWA KUWAKATA NA PANGA KAMA MBOGA MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV
    Next Article NABII GEOR DAVIE AGAWA BAJAJI KWA VIJANA WABADILISHA MAISHA TUMEJENGA NYUMBA NZURI

    Related Posts

    SHEHENA LA MBOLEA ILIYO JAZWA MCHANGA YAKAMATWA WAZIRI ATOA MAAGIZO MAZITO

    March 5, 2023

    Wadau wa Tehama mkoani Arusha watakiwa kutoa ushirikiano kuhakikisha uwepo wa kituo cha ubunifu wa Tehama.

    February 28, 2023

    KATIBU TAWALA MKOA WA ARUSHA ASISITIZA MAFUNZO KUTOKA TUME YA USHINDANI NCHINI

    February 23, 2023

    TANESCO NCHINI KUTEKELEZA MIRADI YA UZALISHAJI UMEME, KUONDOA CHANGAMOTO KWA JAMII

    February 23, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.