Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Michezo»Mzuka Nusu Fainali Chemchem CUP 2022 kuanza leo kuwania mamilion Babati.

    Mzuka Nusu Fainali Chemchem CUP 2022 kuanza leo kuwania mamilion Babati.

    0
    By arushatv on November 2, 2022 Michezo

    Mwandishi wetu, Babati

    Mzuka wa Nusu Fainali ya michuano ya Chemchem CUP 2022, inatarajia kuanza leo, ambapo timu ya Mshikemshike FC ya vilima vitatu itachuana na Timu ya Macklion kutoka kijiji cha Mwada wilaya ya Babati mkoa Manyara

    Michuano hiyo ambayo inashirikisha timu 16 kutoka katika vijiji 10 ambavyo vinaunda jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Burunge zaidi ya sh 25 milioni zinatarajiwa kutumika, ambapo awali timu zote zilipewa seti ya jezi na mipira.

    Nusu fainali ya pili ya michuano hiyo, timu ya Mdori FC ya kijiji cha Mdori itachuana na timu ya Mofuri FC ambayo pia inatoka katika kijiji cha Mdori.

    Michuano hiyo, ambayo inadhaminiwa na Taasisi ya chemchem Association ambayo ni kampuni tanzu ya Chemchem ambayo imewekeza katika eneo hilo la Burunge WMA katika utalii wa picha na hoteli, imekuwa ikifanyika kila mwaka tangu mwaka 2019 lengo za kuzuia ujangili katika eneo hilo na kutunza mazingira.

    Mwenyekiti wa michuano hiyo, Erasto Belela amesema maandalizi yote muhimu ya michezo ya nusu fainali yamekamilika.

    Amesema kabla ya timu hiyo kutinga nusu fainali, timu nyingine zilizofanikiwa kuingia robo fainali ni pamoja na Chui Fc, Manyara FC, Minjingu FC na Olasiti FC ambazo zote zinatoka katika vijiji vilivyounda Burunge WMA.

    Belela amesema licha ya soka pia kutakuwa na michuano ya mpira wa pete ambapo bingwa atazawadia zaidi mbali mbali zinazofikia sh 500,000.

    Katika michuano mwaka huu ni kupiga vita ujangili dhidi ya Twiga ambao umekuwa ukitokea katika eneo hilo.

    Michuano hiyo mwaka huu ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa Manyara,Makongoro Nyerere ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala wa mkoa,Carolina Mtakula.

    Akizundua michuano hiyo alitaka vijana wa Burunge kuwa mabalozi wa kupiga vita ujangili wa katika vijiji vyao.

    mwisho.

    Post Views: 71
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleTAASISI NA WATENDAJI WA TAASISI ZA UMMA WAHAKIKISHE MAZINGIRA WEZESHI YA BIASHARA NA UWEKEZAJI.
    Next Article SERIKALI YAANZISHA KITENGO MAALUM KUSIMAMIA BIASHARA

    Related Posts

    SHABIKI WA KILABU YA YANGA AJITOSA KUMSAPOTI RAIS KWA KUTOA LAKI TANO KWA KILA GOLI

    March 10, 2023

    MR & MISS MAZUBU GRAND HOTEL KUWASHA MOTO MIRERANI

    January 1, 2023

    BONANZA LA MIAKA 5 YA KAMPUNI YA MATI SUPER BRANDS LIMITED NI HISTORIA MANYARA  

    December 30, 2022

    TIMU YA MERVES SPORT CLUB YAFANYA MAUWAJI YAICHAPA 7 KWA 3 MOSHI DC VETERAN

    September 24, 2022

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.