Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»SERIKALI KUFUFUA VIWANDA VILIVYO KUFA NCHINI

    SERIKALI KUFUFUA VIWANDA VILIVYO KUFA NCHINI

    0
    By arushatv on October 18, 2022 Habari

    Na Mwandishi wa A24Tv .

    Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (Mb.) amewahakikishia watanzania kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kufufua viwanda vyote vilivyokufa na kutelekezwa ili viweze kuongeza thamani kwa mazao yanayozalishwa nchini, kutoa ajira
    na kuchangia katika ukuaji uchumi kwa ujumla.

    Waziri Kijaji ameyasema hayo, Oktoba 17, 2022 alipotembelea Kiwanda cha Tumbaku cha Mkwawa kilichopo Mkoani Morogoro kujionea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi baada ya kusimama uzalishajikwa takribani miaka mitatu .

    Aidha, Dkt. Kijaji amewashauri wakulima wa Tumbaku mkoani humo na Tanzania kwa ujumla kulima tumbaku kwa wingi kwa kuwa zao hilo ni la kimkakati na kwa sasa lina soko ambalo ndio kiwanda hicho cha tumbaku kinachochakata zao hilo na kuviuzia viwanda vya kutengeneza sigara.

    Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Bw. Ally Machela amesema kiwanda hicho kuanza kufanya kazi ni neema kwa mkoa huo kwa kuongeza ajira, pato kwa wakulima wa tumbaku na pato kwa taifa.

    Naye Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi katika kiwanda hicho Mhandisi Nicholas Kanyamala amesema kiwanda hicho kilichoanza kazi Septemba 2022, kina Uwezo uliosimikwa wa kuchakata tumbaku tani million 65 kwa mwaka ambapo kwa sasa kinachakata tani mil 8 mpaka 10 kwa mwezi na kimeajili wafanyakazi 800 na mwakani kitaajiri zaidi ya 1,000 na kununua tumbaku ghafi tani million 40.

    Post Views: 150
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleTanzania kuondokana na upungufu wa Sukari 2023
    Next Article MAIPAC na CILAO yabaini utajiri wa maarifa ya asili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutunza Mazingira

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.