Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Makala»PROFESA KIKULA ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA MADINI, TUME YA MADINI NA TGC KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

    PROFESA KIKULA ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA MADINI, TUME YA MADINI NA TGC KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

    0
    By arushatv on October 7, 2022 Makala

    Na Mwandishi wa A24Tv Geita

    Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akiwa ameambatana na Kamishna wa Tume ya Madini, Janet Lekashingo ametembelea banda la Wizara ya Madini, Tume ya Madini na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kwenye Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Bombambili, mjini Geita.

    Katika Banda la Wizara ya Madini alielezwa kuhusu namna Wizara ya Madini inavyoandaa na kusimamia Sera na Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake pamoja na mikakati iliyowekwa katika kuhakikisha watanzania wananufaika na Sekta ya Madini.

    Katika banda la Tume ya Madini elimu ilitolewa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya madini, taratibu za upatikanaji wa leseni za madini nchini, biashara ya madini na taratibu za usalama wa afya na mazingira kwenye migodi ya madini.

    Maeneo mengine ni pamoja na namna watanzania wanaweza kushiriki katika Sekta ya Madini kupitia utoaji wa huduma mbalimbali kwenye migodi ya madini na mchango wa kampuni za uchimbaji wa madini kwenye jamii.

    Aidha Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kilipata fursa ya kueleza majukumu na mikakati yake ya kuhakikisha elimu kuhusu uongezaji thamani inavyofanyika na kuongeza fursa za ajira nchini.

    Post Views: 51
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMAKONDA LEMUTUZ KORTINI KWA UWIZI WA GARI MAGAZETI YA LEO ARUSHA 24TV
    Next Article KIKWETE AFICHUA SIRI LOWASA ALIVYO KOSA URAIS ! MAGAZETI YA LEO A24TV

    Related Posts

    ASKOFU MASANGWA AKOSHWA NA MCHUNGAJI ALIYETUMIKIA KANISA KWA MIAKA34 AMEACHA ALAMA KUBWA

    February 26, 2023

    MZEE MOLLEL AZIKWA KIJIJINI KWAKE WANANCHI WAMWAGA MACHOZI WAZMIA WAKIAGA MWILI WAKE

    February 7, 2023

    WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua zoezi la ugawaji wa vishikwambi 293400 Kwa walimu wote nchini

    November 5, 2022

    PROFESA KIKULA AAINISHA MIKAKATI YA TUME YA MADINI KWENYE UBORESHAJI WA SEKTA YA MADINI

    October 13, 2022

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.