Site icon A24TV News

MKURUGENZI MTENDAJI WA SOTTA MINING, DAMIEN VALENTE AIPONGEZA WIZARA YA MADINI, TUME YA MADINI KWA UTOAJI WA HUDUMA BORA

Na Mwandishi wa A24Tv .

Mkurugenzi Mtendaji wa Sotta Mining, Damien Valente amepongeza huduma zinazotolewa na Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini hususan utoaji wa leseni na usimamizi wa biashara ya madini kupitia masoko na vituo vya ununuzi wa madini vilivyoanzishwa nchini.

Valente amesema hayo leo Oktoba 03, 2022 mara baada ya kutembelea Banda la Tume ya Madini na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) katika Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili mjini Geita .

” Nitumie fursa hii kuipongeza Wizara ya Madini kwa kuweka Sheria bora na Tume ya Madini kwa huduma nzuri lengo likiwa ni kuhakikisha Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi, na sisi kama wawekezaji tupo tayari kushirikiana na Serikali kwa maendeleo endelevu kwenye Sekta ya Madini,” amesema Valente