Site icon A24TV News

Makamu wa Rais Zanzibar Anena kuelekea Uzinduzi wa Matokeo ya Sensa

Na Doreen Aloyce, Dodoma

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Mohamed Abdullah amesema kufuatia kuwepo kwa uzinduzi wa matokeo ya awali ya sensa ya watu na makazi ya mwaka huu unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan imefikia asilimia 85.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wakati alipotembelea kukagua uwanja wa Jamhuri ambapo kutafanyika uzinduzi huo mnano oktoba 31 mwaka huu ambapo utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali.Aidha ali

Aidha amefafanua kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na hali iliyopo inavyoonekana imefikia zaidi ya asilimia 85 kilichobaki ni kukamilisha mambo madogo madogo na kitakachobaki ni ile siku ya shughuli ya watanzania kuhudhuria kwa mujibu wa utaratibu,

”Rais Samia atazindua matokeo ya mwanzo ya sensa ya watu ya mwaka 2022 na tumejipanga vizuri na tunaamini kwamba uzinduzi huu utakuwa wa kisasa na hafla hiyo itakuwa mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari na watanzania watapata nafasi ya kuona na kusikia.”amesema Abdallah

“Sensa ya mwaka huu ni ya kisasa na ya kipekee sababu imefanyikia kidigitali kuliko sensa za awamu Zote na takwimu hizi zitatusaidia katika maendeleo mbalimbali ya kiuchumi, haitatumika Tanzania pekee bali itatumika kwa nchi nyingi duniania kwakuwa tumekuwa tukishirikiana na nchi mbalimbali katika mambo tofauti tofauti,”amesema.

Ameongeza kuwa takwimu za matokeo ya sensa zitasaidia Kwa kiasi kikubwa shughuli za kiuchumi na kijamii ili kupanga maendeleo kwa maslahi ya Taifa.

Kwa mujibu wa Makamu huyo wa Rais amesema kuna vigezo ambavyo vinachukuliwa kimataifa vya ubora wa sensa na hayo yatatoka taarifa zake baada ya uzinduzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Maandalizi ya hafla hiyo Rosemary Senyamule amesema maandalizi ya yanaendelea vizuri kwani watu wako kazini muda wote.

Amesema katika kuhakikisha kila kitu kinafanikiwa kwa weledi na wameunda kamati zipatazo 11 zinazoongozwa na Wakuu wa Wilaya

Senyamule amesema kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa na vyombo vingine wamehakikisha suala hilo linapewa kipaumbele siku hiyo ya tukio.

“Kiujumla tuko vizuri tumeunda kamati 11 na zinaongozwa na wakuu wa Wilaya, kubwa zaidi ni kuhakikisha wanawahamasisha wananchi katika maeneo yao siku hiyo wafike uwanjani mapema kwa ajili ya kukamilisha zoezi Hilo,”Amesema Senyamule

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kongwa ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya itifaki na mapokeze Remedius Mwema amesema kuwa mpaka sasa tayari mabalozi kutoka Nchi mbalimbali wamethibitisha kushiriki katika zoezi hilo.

Amesema bado wanaendelea kutoa mialiko ya viongozi watakao hudhuria na wageni kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwemo viongozi na wananchi zaidi ya 140.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi jijini Dodoma wamesema kuwa wamejipanga vyema kumpokea Rais kwa shangwe na nderemo ili kuweza kuzindua matokeo hayo.

Wamesema kuwepo kwa ugeni huo ni fursa kwa wakazi wa Dodoma kwani wanaenda kufanya biashara zao ambazo zitawaingizia kipato na Taifa kwa ujumla kupitia kodi.

Mwisho.