Site icon A24TV News

WAZIRI KIJAJI SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHRA NCHINI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini (Blueprint) ili kuvutia uwekezaji na kuwezesha ufanyaji biashara wenye tija utaokuza uchumi wa taifa kwa ujumla.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo  wakati  alipokutana na kufanya mazungumzo na
Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika anayeshughulikia Ukuzaji wa Uchumi na Taasisi kutoka Benki ya Dunia (WB), Dr.Asad Alam na ujumbe wake kuhusu fursa za uwekezaji na ufanyaji biashara zilizopo Tanzania. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara jijini ……. Septemba 29, 2022.

Akiwa ameambata na Viongozi wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara akiwemo Naibu Katibu Mkuu  Dkt. Hashil Abdallah, Dkt. Kijaji amemhakikishia Mkurugenzi huyo kuwa Serikali iko tayari kushirikiana na Benki ya Dunia kuanzisha na kuendeleza programu mbalimbali za kuwawezesha wajasikiamaki wadogo na wa kati kuwekeza na kufanya biashara ili kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.

Aidha, Dkt. Kijaji amesema Serikali inaendelea kufanya mamoresho mbalimbali kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini ( Blueprint) ikiwemo kupitia na kurekebisha sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Uwekezaji pamoja na kupunguza tozo mbalimba ambazo zimekuwa kikwazo katika ufanyaji biashara na uwekwzaji.

Naye Mkurugenzi huyo wa Kikanda chini ya Benki ya Dunia amesema Programu hiyo ya kukuza uchumi na Taasisi amesema Benki dunia kupiyia programu hiyo iko tayali kuwawezesha wajasilimali watanzania katika sekta mbalimbali kuendeleza biashara zao zitakazoongeza ajira, pato la Taifa na kuleta maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi kwa ujumla.

Matukio Katika Picha ya pamoja Mkurugenzi wa Kikanda chini ya Benki ya Dunia ,.Asad Alam na Mh Waziri Ashantu Kijaji .