Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Makala»TUME YA MADINI YAENDELEA KUWANOA WACHIMBAJI WA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

    TUME YA MADINI YAENDELEA KUWANOA WACHIMBAJI WA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

    0
    By arushatv on September 28, 2022 Makala

    Na Mwandishi wa A24Tv Geita

    _Wapongeza kasi ya utoaji elimu._

    Wataalam kutoka Tume ya Madini wameendelea kutoa elimu kwa wachimbaji  wa madini kutoka katika mkoa wa Geita na mikoa ya jirani katika Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili mjini Geita .

    Elimu imetolewa katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya madini, taratibu za upatikanaji wa leseni za madini nchini, biashara ya madini na taratibu za usalama wa afya na mazingira kwenye migodi ya madini.

    Maeneo mengine ni pamoja na namna watanzania wanaweza kushiriki katika Sekta ya Madini kupitia utoaji wa huduma mbalimbali kwenye migodi ya madini na mchango wa kampuni za uchimbaji wa madini kwenye jamii.

    Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi waliotembelea banda la Tume ya Madini wamepongeza  weledi wa wataalam wa Tume ya Madini kwenye utoaji wa elimu na kuwaomba kuendelea na zoezi hilo katika mikoa mingine yenye shughuli za uchimbaji wa madini.

    Akizungumza kwenye maonesho hayo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Tume ya Madini, Greyson Mwase amesema kuwa wamejipanga kutoa elimu kwa wadau wa madini na wananchi wote wanaotembelea maonesho hayo pamoja na huduma kama vile upimaji wa madini na kuwaelekeza namna ya kujisajili katika mtandao wa leseni za madini (online mining cadaster transactional porta).

    Matukio katika picha maonyesho yakiendelea

    “ Tumejikita pia kutoa elimu katika eneo la ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini (local content) ili wananchi wengi waweze kufahamu fursa zilizopo kwenye migodi ya madini na kuchangamkia kama vile utoaji wa huduma za vyakula, vifaa vya usalama migodini, ulinzi ili nao waweze kunufaika,” amesema Mwase.

    Ameendelea kusema kuwa Tume imeendelea kuweka mikakati mingine ya kuelimisha umma ikiwa ni pamoja na uandaaji na urushaji wa vipindi vya redio na televisheni, tovuti na mitandao ya kijamii.

    Post Views: 37
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleCCM YAFUTA CHAGUZI 5 VIGOGO WAANGUKIA PUA ! MAGAZETI YA LEO ARUSHA 24TV
    Next Article ZIARA YA MBIBO KWENYE BANDA LA TUME YA MADINI KATIKA MAONESHO YA MADINI GEITA

    Related Posts

    ASKOFU MASANGWA AKOSHWA NA MCHUNGAJI ALIYETUMIKIA KANISA KWA MIAKA34 AMEACHA ALAMA KUBWA

    February 26, 2023

    MZEE MOLLEL AZIKWA KIJIJINI KWAKE WANANCHI WAMWAGA MACHOZI WAZMIA WAKIAGA MWILI WAKE

    February 7, 2023

    WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua zoezi la ugawaji wa vishikwambi 293400 Kwa walimu wote nchini

    November 5, 2022

    PROFESA KIKULA AAINISHA MIKAKATI YA TUME YA MADINI KWENYE UBORESHAJI WA SEKTA YA MADINI

    October 13, 2022

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.