Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»MKAKATI WA KUTANGAZA UTALII KUSINI MWA TANZANIA WAZINDULIWA Mom September 26, 2022

    MKAKATI WA KUTANGAZA UTALII KUSINI MWA TANZANIA WAZINDULIWA Mom September 26, 2022

    0
    By arushatv on September 26, 2022 Habari

    Na Emmanuel mkulu

    Njombe

    Serikali chini ya wizara ya Maliasili na utalii nchini Tanzania imetangaza rasmi mikakati mbalimbali ya kuendeleza sekta ya utalii inayochangia pato la taifa kwa asilimia 17.

    Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa kutangaza utalii kusini mwa Tanzania Waziri wa maliasili na utalii Balozi Dokta Pindi Chana akiwa mkoani Njombe amesema wizara imeweka wazi mikakati mbalimbali ikiwemo kutangaza utalii kusini mwa nchi,Utamaduni,pamoja na fursa za utalii zilizopo katika mikoa husika.

    Wabunge wa majimbo ya Makambako Deo Sanga,Ludewa Joseph Kamonga na Makete Festo Sanga Wamesema ili fursa ya utalii kusini mwa Tanzania iweze kufanikiwa kwa akali kubwa kunahitajika kuboreshwa kwa miundombinu ya barabara,Viwanja vya ndege pamoja na kuendeleza mambo ya asili yaliyopo.

    Awali mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema ifike wakati baridi iliyopo Njombe iwe fursa kwa kuwaingizia kipato wananchi na taifa ikiwa njia moja wapo ya kuutangaza utalii nchini kauli iliyoungwa mkono na Mkuu wa mkoa wa Lindi Zainabu Teleck kwa niaba ya wakuu wa mikoa tisa ya kusini mwa Tanzania.

    Baadhi ya wananchi mkoani Njombe akiwemo Adili Nguhula na Dokta Florian Mtei mdau wa Utalii nchini wamekiri kuwa mpango huo utakwenda kusisimua utalii kusini mwa Tanzania.

    Post Views: 63
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMsitu Uliotunzwa Zaidi Ya Miaka 800 Wa NYUMBANITU Waingia Kwenye Orodha Ya Vivutio mhimu Mkoani Njombe
    Next Article PADRI ABAKA WATOTO 10 KILIMANJARO ,ASOMEWA MASHTAKA 3 MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.