Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Uncategorized»DC ARUSHA AHAMASISHA CHANJO YA POLIO, KWA WATOTO ASEMA NI CHANJO YA MATONE SIO SINDANO.

    DC ARUSHA AHAMASISHA CHANJO YA POLIO, KWA WATOTO ASEMA NI CHANJO YA MATONE SIO SINDANO.

    0
    By arushatv on August 29, 2022 Uncategorized

    Na Geofrey Stephen. Arusha

    Mkuu wa wilaya ya Arusha,Said Mtanda amewataka wazazi wote wilayani hapa kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kwenye vituo vya afya na zahanati ifikapo Septemba Mosi mwaka huu ili wakapatiwe chanjo ya ugonjwa wa Polio .

    Mtanda ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wajumbe mbalimbali wa kamati ya chanjo ya Polio jijini Arusha.

    Akizungumza katika kikao hicho Mtanda alisema kuwa ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha anampeleka mtoto wake aliye chini ya umri wa miaka mitano katika zahanati au kituo cha afya ifikapo tarehe hiyo ili aweze kupata chanjo hiyo ambayo inalenga kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Polio.

    Mtanda alisema kwamba chanjo ya polio inatolewa kwa matone na sio sindano kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na kuwaondoa hofu wakazi wa Arusha kwamba haina madhara yoyote.

    “Serikali haiwezi kuleta chanjo yenye madhara nawahimiza wazazi wote ifikapo Septemba mosi mpaka nne wahakikishe wanawapeleka watoto wao kwenye vituo vya afya na zahanati wakapate chanjo ya polio “alisema Mtanda

    Naye mwenyekiti wa kamati ya chanjo jijini Arusha,Florence Solomon alisema kuwa maandalizi mpaka sasa maandalizi ya zoezi la utoaji wa chanjo hiyo linaenda vizuri na kazi iliyobaki ni kupeleka elimu kwa wananchi.

    Mwenyekiti huyo amesema kwamba baadhi ya wananchi bado wanafikiri ya kwamba chanjo itakayotolewa ni ile ya UVIKO-19 na kuvitaka vyombo vya habari kujikita kutoa elimu ya kutosha juu ya chanjo ya Polio.

    “Tupeleke elimu kwa wananchi wengi kwa kuwa kuna baadhi ya watu wanadhani chanjo ya Polio ni ya UVIKO-19 waandishi wa habari mtusaidie kwa hili “alisema Solomon

    Mratibu wa chanjo hiyo jijini Arusha,Hashim Mtiti kwa sasa maandalizi yote ya utoaji wa chanjo hiyo yamekamilika na kazi iliyobaki ni kupeleka hamasa kwa jamii.

    Mtiti alisema kwamba kuna ushirikishwaji mkubwa sana katika zoezi hilo la utoaji wa chanjo ya polio kupitia makundi mbalimbali na safari hii wanatarajia kuvuka lengo kwa asilimia 100.

    Mwisho

    Post Views: 150
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleNCCR MAGEUZI WAMVAA MUTUNGI ATUMTAKI ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV .
    Next Article BILIONEA KAWISHE AFUNGUKA MAZITO,AELEZA KUTUMIA ZAIDI BIL 1 KUHUDUMIA MGODI WAKE ,ASEMA HAAMINI KATIKA USHIRIKINA.

    Related Posts

    SHEHENA LA MBOLEA ILIYO JAZWA MCHANGA YAKAMATWA WAZIRI ATOA MAAGIZO MAZITO

    March 5, 2023

    Wadau wa Tehama mkoani Arusha watakiwa kutoa ushirikiano kuhakikisha uwepo wa kituo cha ubunifu wa Tehama.

    February 28, 2023

    KATIBU TAWALA MKOA WA ARUSHA ASISITIZA MAFUNZO KUTOKA TUME YA USHINDANI NCHINI

    February 23, 2023

    TANESCO NCHINI KUTEKELEZA MIRADI YA UZALISHAJI UMEME, KUONDOA CHANGAMOTO KWA JAMII

    February 23, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.