Site icon A24TV News

Wizara ya Maliasili na Utalii imejipanga kushirikiana na Wadau  wa sekta binafsi kujadili mapendekezo ya sera,

Na Geofrey Stephen . ARUSHA.

SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imejipanga kwakushirikiana na Wadau  wa sekta binafsi kujadili mapendekezo ya sera, Sheria, Taratibu na kanuni kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika sekta ya utaliinchini .

Aidha Serikali imejipanga kuhakikisha inatengeneza mfumo wa pamoja wa biashara baina ya wadau wa Utalii ikiwa lengo ni kupata.

huduma zote sehemu moja za tozo kodi na malipo yote ya sekta hiyo(Onestop Shop) ili sekta hiyo ichangie kikamilifu katika uchumi

Akiongea wakati akifungua mkutano wa Wadau wa sekta ya Utalii (MPPD) Jijini Arusha Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt,Pindi Chana

alisema kwamba maagizo aliyotoa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa 13 wa baraza la taifa la biashara TNBC jijini Dodoma alituagiza tukutane na sekta binafsi hususani sekta ya Utalii kujadili mapendekezo na mageuzi ya sera sheria kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara hiyo.

Alisema kwamba serikali imedhamiria kwa dhati kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika sekta ya Utalii ili ichangie kikamilifu

katika uchumi na maendeleo ya Taifa letu kwa ujumla pia dhamira hiii naenda sambamba na uendelezaji wa malengo ya kimkakati ya mpango wa Tanzania The Royal Tour katika kukuza Utalii kadhalika na Uhifadhi wa maliasili na malikale zetu.

Awali akiongea wakati akimkaribisha Waziri Chana  katika kikao hicho

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Eliaman Sedoyeka alisema kwamba kupitia wizara hiyo wamejipanga kuongeza juhudi kubwa za kuutangaza Utalii duniani ikiwa ni ishara ya kuunga juhudi za Rais

Samia Suluhu Hassan aliyoyafanya kwa vitendo kuandaa Filamu ya RoyalT our.

Alisema Pamoja na sekta hiyo kuathiriwa na uwepo wa janga la Uviko 19

sanjari na vita baina ya mataifa ya Urusi na Ukrein bado wizarai taendelea kupanua soko la utalii kufikia malengo ya watalii milion 5 mwaka 2025.

Kwa Upande wake Mshauri wa Mazingira ya Uwekezaji IFC Anita Kundy alisema kwamba Tangu 1956, IFC imewekeza zaidi ya dola bilioni 2.8

katika miradi zaidi ya 260 katika nchi 89 na zaidi ya nusu yau wekezaji huu katika nchi nyingine. Nchini Tanzania, tumewekeza pia katika hoteli jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Dunia na Baraza la Utalii, kila dola inayotumika kwau safiri na utalii inazalisha zaidi ya dola tatu za pato la kiuchumi.

Zaidi ya wafanyakazi milioni 100 wameajiriwa katika sekta hii duniani

kote, na mapato ya utalii yanachangia mtiririko wa fedha zaidi kwan chi zinazoendelea kuliko mtiririko wote wa misaada kutoka kwaw afadhili wa kigeni.

Alisema IFC inafuraha kuunga mkono na kusapoti kufikiwa kwa malengo

muhimu ya serikali ya awamu ya 6 ya kuifanya Tanzania kama kivutio cha

utalii na uwekezaji. Kwa miaka sitini, IFC, mwanachama wa Benki ya

Dunia, imefanyakazi na sekta binafsi kwenye kuleta masuluhishoy aliyoleta mabadiliko chanya kijamii na kiuchumi.

Kwa Mujibu wa Kundy imefanikisha kuunda masoko mapya,

kuhamasisha wawekezaji binafsi, na kutoa msaada wa kitaalamu. IFC

inawekeza katika hoteli na utalii kwasababu ya faida zake kubwa za

maendeleo, hasa kwa nchi za kipato cha chini na zilizoathiriwa na migogoro.

Ends…..