Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»WAZIRI WA JANUARY MAKAMBA AZINDUA BODI YA TPDC ASISITIZA UCHAPAJI WA KAZI

    WAZIRI WA JANUARY MAKAMBA AZINDUA BODI YA TPDC ASISITIZA UCHAPAJI WA KAZI

    0
    By arushatv on July 4, 2022 Habari

    Waziri wa Nishati January Makamba amesema uendeshaji umahiri na umadhubuti wa uongozi wa shirika la TPDC, ni Jambo ambalo serikali unalipa uzito wa hali ya juu.

    Waziri January Makamba  Akipitia Makabrasha ya Kikao hicho.

    Makamba Ameyasema hayo wakati akizindua bodi ya wakarugenzi wa shirika hilo jijini Arusha na kueleza kwamba uteuzi wa bodi hiyo unaakisi dira na Malengo mapya ya serikali kwa shirika hilo kuelekea katika mafuta na gezi.

    Amesema bodi hiyo chini ya mwenyekiti wake balozi Ombeni Sefue inakidhi nafasi ya TPDC katika maendeleo ya nchi, Dira na mwelekeo mpya wa TPDC katika uchumi mpya wa Gesi na maendeleo ya mafuta nchini kwa ujumla.

    “Dhamira yetu ni kuona shirika hili linatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi na sio katika mapato tu bali uendeshaji wa rasilimali watu katika tasnia hii lakini pia ushiriki wa nchi katika miradi mikubwa ya kimkakati ya mafuta na Gesi” Alisema Makamba

    Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi hiyo ya TPDC Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni katibu mkuu Kiongozi mstaafu amesema wao kama bodi kazi yao ni kwenda kuchangamsha na kuhakikisha kila kitu kinaenda inavyotakiwa na sekta hii ili taifa liweze kunufaika na rasilimali zake za mafuta na Gesi tulizopewa na Mungu.

    Mikakati iliyopo kwa sasa ni ile ya serikali na haijaanza leo tutaipitia kama bodi mpya tumefanikiwa wapi na changamoto ni zipi na zitatatuliwaje ili kazi iendelee vizuri kujenga TPDC yenye kusaidia serikali.

    Awali Mkurugenzi wa Shirika la mafuta na Gesi nchi muhandisi James Maragio amesema kuwa miradi ya mafuta na Gesi itakapokamilika itasaidia kutatua changamoto za wananchi.

    Picha ya pamoja ya wajumbe ya bodi iliyo zinduliwa na Mh waziri Makamba jijiji Arusha

    Alisema kuwa wana miradi mikubwa ikiwemo mradi wa bilion 40 ikiwemo mradi wa kujenga bomba la mafuta kutoka hoima Uganda ambao umeonyesha mafanikio pia kuna maradi wa kutafuta mafuta katika bonde la ufa ambao upo kwenye Mchakato.

    Post Views: 90
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleSHILINGI BILLIONI 8 KUZALISHA MADAKTARI BINGWA MAGAZETI YA LEO NA A24TV
    Next Article KIPANGA AZINDUA SHULE YA KIMATAIFA JUMUISHI YA MFANO YA SEKONDARI PATANDI ARUSHA.

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.