Site icon A24TV News

WATOTO WA NNE WALIO FARIKI DUNIA KWA KUNYWA SUMU VIPIMO VYAFIKA KWA MKEMIA MKUU

Na Joseph Ngilisho Arusha

Vifo vya utata kwa watoto watano wa familia moja waliofariki kwa kufuatana, wakazi wa kijiji cha Mswakini  wilaya ya Monduli,mkoani hapa,uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa ,marehemu hao walikula ama kunywa kimiminika chenye sumu.

Aidha wataalamu wa maabara katika hospitali  ya mkoa Mt.Meru tayari wamechukua Sampuli za marehemu kwa ajili ya kupelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali ili kubaini chanzo halisi juu ya vifo vya marehemu.

Akiongea na vyombo vya habari wakati wa kuagwa kwa miili ya marehemu wanne katika hospitali  ya Mkoa Mt Meru,jijini hapa,mkuu wa wilaya ya Monduli ,Frank Mwaisumbe alibainisha kuwa uchunguzi wa awali ,marehemu wamekutwa na viambata vyenye sumu katika miili yao.

Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya amepiga marufuku matumizi ya dawa za miti shamba zisizothibitishwa kitaalamu akidai ndio chanzo cha vifo visivyona ulazima na kuitaka jamii hiyo kutumia dawa za kienyeji zilizothibitishwa.

Alisema kuwa marehemu hao,walifariki kwa nyakati tofauti baada ya kuvimba matumbo na macho kuwa ya njano ,jambo  linaloashiria walikula kitu kibaya lilichowasababishia madhara.

Aliwataja marehemu hao kuwa ni ,Lemali Nyangusi(8)Sophia Nyangusi(5),Lenendoye Nyangusi (8)na Veronica  Nyangusi (11)Lopoi Nyangusi (6)ambaye alikuwa wa kwanza  kufariki na kuzikwa wote wakiwa wakati za Mswakini Chini ,Makuyuni wilayani Monduli.

Hata hivyo mkuu hiyo wa wilaya alisema kuwa wazazi wa marehemu ,Nyangusi Mollel(45) na Nangoye Nyangusi(32)wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa uchunguzi wa tukio hilo.

Alifafanua  kuwa chanzo cha tukio hilo ni marehemu hao kudaiwa kunywa maziwa yanayosadikiwa  kuwa na sumu ambapo baada ya kuyatumia walianza kujaa na kuvimba matumbo ndipo walipopelekwa katika kituo cha afya cha kijeshi TMA,wilayani Monduli na baadaye kuhamishiwa katika hospitali ya rufaa,Mount Meru walikofikwa na mauti.

Mmoja ya wanafamilia hiyo,Kilanian Lendoya alisema kuwa tukio lilianza mnamo.julai Mosi mwaka huu ambapo mtoto mmoja wapo Lopoi Nyangusi (6)aliugua na kupoteza hafamu na kupelekwa katika katika hospitali  moja wapo iliyopo wilayani karatu.

Alisema siku ya tano,Julai 5 mwaka huu akiwa amelazwa katika  hospitali hiyo alifariki dunia na kuzikwa nyumbani kwao Mswakini.

Alisema alisema kuwa baba yao Nyangusi  Mollel mwenye watoto saba,watoto wengine wanne waliendelea kuumwa na ilipofika julai 16 walipelekwa katika kituo cha afya cha jeshi la wananchi Tanzania TMA Monduli .

Alisema kuwa Julai 17 walitolewa hospitalini kwa ajili ya kupelekwa maombi kuombewa kutokana na ugonjwa wanaoumwa kutojulikana , lakini ghafla hali zao zilibadilika na kupelekwa katika hospitali ya mkoa Mount Meru ambapo walifariki dunia kwa kupokezana.

Marehemu hao wamesafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwao Mswakini Chini huko wilayani Monduli.

Ends…