Site icon A24TV News

UGONJWA WA SARATANI BADO TISHIO NCHINI TAKWIMU ZAONGEZEKA

Na Geofrey Stephen Arusha

SERIKALI imeeleza kwamba katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ugonjwa ya Saratani umeongezeka na kuwa tishio hapa nchini ambapo takwimu za mwaka jana 2021 zikionesha wagonjwa wapatao 14,136 waligundulika kuwa na Saratani ukilinganisha na mwaka 2020  wagonjwa walikuwa 12,000 tu.

Akizungumza katika kongamano la sayansi la Saratani, jijini hapa,Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Saratani Ocean Road dkt Julius Mwaiselage ,ambaye alimwakilisha waziri wa afya ,Ummy Mwalimu,aliwataka wataalamu kutumia jitihada mbalimbali katika kudhibiti ugonjwa huo ambao unatishia mustakabali wa maisha kwa watanzania.

Alisema magonjwa ya Saratani yanachangiwa zaidi na aina mbalimbali za maisha ikiwemo,ulaji usiofaa, kutofanya mazoezi ,unene uliokithiri na matumizi ya tumbaku.

Azungumzia takwimu za kiduniani zilizofanywa na shirika la kimataifa la tafiti za Kansa AYAC ,zimeeleza kwamba kila mwaka wagonjwa milioni18,000 wanapata ugonjwa wa Saratani na wagonjwa milioni 9.6 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa huo na wagonjwa milioni 43.8 wanaishi na saratani.

“Ulaji usiofaa na kutofanya mazoezi kwa kiasi kikubwa inachingia kupata magonjwa yasioambukizi ikiwemo Saratani Shinikizo la Damu na hata kisukari hivyo Watanzania wametakiwa kujenga tabia ya kupima afya za mara kwa mara”Alisema

 

Kwa Muktadha huo Madaktari  bingwa wa saratani kutoka nchi mbalimbali wamekutana mkoani Arusha kwa lengo la kujadili na kubadilishana uwezo wa namna gani wanaweza kuboresha huduma za matibabu ya saratani ikiwemo maeneo ya vijijini.

Amesema kwamba ndio maana serikali kwa Sasa imejipanga kila Kanda kuweka mashine za ST SCAN ikiwa ni mkakati wa upimaji wa Mapema kungundua tatizo hilo na kuchukuwa hatua za haraka za matibabu kwa wale watakaogindulika.

“Serikali inafanya kazi changamoto zote ikiwemo kuweka mashine za ST scan katika hospitali za Kanda kwani katika kipindi Cha miaka 10 ikiwemo miaka miwili ya hivi karibuni zaidi ya wagonjwa 7000 wapya wameandikishwa hivyo kuonyesha kukua kwa kasi nchini”


Aidha ametoa rai kwa wananchi  kuweza kutumia Fursa mbalimbali  ambazo serikali inazitoa kwa  kuwa na tabia ya kupima huku akiwataka wanaume kujitokeza kwa wingi kupima tezi dume na pindi mtu atakapobainika na changamoto hiyo aweze kupatiwa tiba mapema.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Madaktari bingwa wa saratani Jerry Ndumbalo ameitaka serikali kuangalia namna bora ya kuongeza wigo mpana wa madaktari bingwa ili kuweza kupambana na saratani nchini angali Mapema.

Kwa Mujibu wa Dkt.Ndumbaro amebainisha kwa sasa wana madaktari bingwa 38 huku idadi ya wagonjwa inaongezeka kwa kasi  kwani hivi sasa kwa mwaka wanaandikisha wagonjwa wapya takribani elfu saba  huku kiataalamu daktari mmoja anatakiwa kutibu wagojwa mia moja.

Alisema kwamba serikali ya awamu ya sita imeleta mashine za kisasa za mionzi katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ikiwa Lengo ni kuongeza upimaji ambapo aliwataka wanaume kujitokeza kwa wingi kupima tezi dume kwani imeonekana wagonjwa huo kupanda kwa miaka ya karibuni.

“Miaka ya nyuma Saratani ya Tezi dume haikuwepo ila Sasa imepanda hadi nafasi ya nne ikiwemo Saratani ya utumbo ambayo nayo haikuwepo hapo awali katika chati niwaombe sana wanaume mwitikio wenu sio mzuri katika zoezi la upimaji wa Saratani ya Tezi dume”

Ulaji wa vyakula fast food ikiwemo chips, soda , na vyakula ambavyo havijaandaliwa vizuri na mtindo wa maisha unaopelekea kutokufanya mazoezi unachangia kwa kiasi kikubwa kupatwa na magonjwa yasiyo ambukizwa hivyo wananchi wanashauriwa kupima afya mapema ili kuweza kupatiwa matibabu pindi wanapogundulika na changamoto hizo  za saratani.

Ends…