Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»TANZANIA YAUZA TAN 10000 YA NYAMA BARA LA ASIA KWA MIEZI SITA

    TANZANIA YAUZA TAN 10000 YA NYAMA BARA LA ASIA KWA MIEZI SITA

    0
    By arushatv on July 6, 2022 Habari

    Na Ahmed Mahmoud

    Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mashamba Ndaki ameeleza kwamba katika kipindi cha miezi sita Tanzania imeuza nyama tani elfu 10 katika nchi za Bara la Asia tofauti na miaka ya nyuma na huenda Mwaka huu ikauza zaidi ya miaka yote.

    Ndaki ameyasema hayo jijini Arusha wakati ya akifungua warsha ya siku saba ya wataalamu wa sekta ya mifugo kutoka nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika{SADC} unaolenga kujadili namna ya kuongeza thamani ya nyama nyekundu yanayotokana na ng’ombe wa asili.

     

    Amesema kuwa, ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan katika nchini za Bara la Asia hususani nchi za kiarabu imeweza kufungua mwanga kwa nchi hizo kuwa wanunuzi wakubwa wa nyama ya hapa nchini na hadi kufikia Desemba mwaka huu huenda Tanzania ikauza nyama nyingi kuliko miaka yote.

    Waziri Ndaki amesema kuwa,kutokana na hilo kupitia Wizara yake wamepanga mpango kazi wa kuhakikisha wanafuga mifugo bora yenye lengo la kumpatia mlaji bidhaa bora kwa maslahi ya nchi.

     

    “katika kipindi cha mwaka mzima wa mwaka jana Tanzania iliuza nje ya nchi nyama tani Elfu 7 lakini kwa mwaka huu hali imekuwa tofauti sana kwani katika kipindi cha miezi sita nchi imefanikiwa kuuza nje ya nchi nyama ya kiasi cha tani Elfu 10.”amesema Waziri Ndaki.

     

    Waziri amesema kuwa, kutokana na hali hiyo Wizara imepanga kuboresha sekta ya Mifugo kwa kufuga kisasa katika vituo vyake vya ng’ombe na mbuzi kuwa na mifugo yenye ubora itakayoshindana na soko na huku akiwataka wafugaji kufanya hivyo kwa maslahi ya nchi.

     

    Amesema kuwa, katika kuboresha hilo Wizara imepanga kujenga mabwawa ya Mifugo zaidi katika Mikoa yote yenye mifugo mingi, pamoja na kujenga majosho kwa ajili ya kulinda ugonjwa kwa mifugo.

     

    Waziri Mashimba ameongeza kuwa serikali imepanga kushirikiana na nchi za SADC katika kuboresha mifugo na kuwa na nyama bora kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi kwani nchi za SADC zina mifugo bora kuliko nchini zingine katika Bara la Afrika.

     

    Mtaalamu wa maswala ya teknolojia ,ujuzi na ubunifu katika mradi wa Live2Afrika (AU-IBAR)Dk Mary Kariuki amesema kuwa,wamekuwa na mijadala ya kutosha katika eneo hilo katika kuhakikisha wanaboresha mnyororo wa nyama wa thamani katika eneo la kimazingira katika nchi za ukanda wa SADC.

    Naye Kaimu Mkurugenzi wa Muungano wa Afrika kwa rasilimali za Wanyama(AU -IBAR) Dk .Nick Mwankpa amesema kuwa, wataalamu wa nchi hizo watatoka na maazimio yenye tija kwa nchi hizo na kwenda kufanyiwa kazi kwa ajili ya faida ya nchi hizo na sio vinginevyo.

    Dk Mwankpa alisisitiza kuwa Lengo la warsha hiyo ni kuongeza thamani ya mazao ya mifugo barani Afrika ili wafugaji waweze kunufaika na Rasilimali zao na kuondoa Utamaduni wa kumiliki mifugo mingi pasipo kuwa na faida.

    Post Views: 71
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleSHULE ZA SERIKALI KIDEDEA MATOKEO KIDATO CHA 6 MAGAZETI YA LEO NA A24TV
    Next Article PANYA TISA WAANZA MAFUNZO KUPAMBANA NA WALIOPATA MAJANGA NA MAGONJWA

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.