Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»SAKATA LA GARI LA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA LILILOSHIKILIWA KWA MADAWA YA KULEVYA LAIBUKA TENA KWENYE KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI.

    SAKATA LA GARI LA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA LILILOSHIKILIWA KWA MADAWA YA KULEVYA LAIBUKA TENA KWENYE KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI.

    0
    By arushatv on July 27, 2022 Habari

    Moses Mashalla,

    Sakata la gari lililoshikiliwa kwa tuhuma za kubeba madawa ya kulevya limeibuka tena ndani ya kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Jiji la Arusha kilichofanyika leo katika ukumbi wa jiji.

    Gari hilo lenye nambari STJ 7333 lilishikiliwa mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu na jeshi la polisi wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro likiwa na shehena ya mirungi ambapo linashikiliwa mpaka sasa.

    Akiibua hoja hiyo ndani ya kikao hicho diwani wa kata ya Ngarenaro,Isaya Doita aliuliza nini hatma ya gari hilo ambalo lilikamatwa likiwa na shehena ya mirungi.

    “Mheshimiwa Mwenyekiti gari hili mpaka sasa linashikiliwa na hatujui linarejeshwa lini tunaomba kupata ufafanuzi “alisema Doita

    Akijibu swali hilo afisa utumishi wa jiji la Arusha,Gerald Ruzika alisema kuwa mpaka sasa gari hilo bado linashikiliwa na polisi wilayani Rombo kama kielelezo na derava wake yuko rumande na kuwataka madiwani waendelee kuwa na subira.

    Katika hatua nyingine Meya wa jiji la Arusha,Maximillan Iranqe alifafanua suala la uwekaji wa taa za barabarani pembezoni mwa hoteli yenye hadhi ya nyota 5 ya Grand Melia na kusema kuwa tayari maandalizi ya uwekaji wa taa hizo yanaendelea.

    Meya huyo alifafanua kuwa jiji la Arusha kwa kushirikiana na uongozi wa hoteli hiyo wanatarajia kuweka taa hizo pembezoni mwa barabara inayopita hotelini hapo kwa lengo la kuimarisha usalama.

    “Grand Melia ni hoteli yenye hadhi ya nyota 5 lazima tuipe kipaumbele hivyo tutashirikiana nao kwa kuweka taa hizo kuimarisha usalama “alisema Meya Iranqe

    Mwisho…

    Post Views: 87
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleYANGA na Sportpesa zasaini Mkataba mpya wa Udhamini
    Next Article WAZEE WA KIMILA VIONGOZI WA DINI WAAPA KUHAMASISHA SENSA NA MAKAZI MKOANI ARUSHA

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.