Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»RUWASA yaleta faraja wakazi Msomera

    RUWASA yaleta faraja wakazi Msomera

    0
    By arushatv on July 11, 2022 Habari

    Mwandishi wa A24Tv, Handeni

    Wakala wa Maji na usafi wa mazingira Vijijini(RUWASA) imeleta faraja Kwa wakazi 17,000 wa kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga Kwa kuwapata maji safi na Maji ya Mifugo .

    RUWASA inatumia zaidi ya sh 3 bilioni Kwa sasa katika miradi ya maji Msomera Kwa kusambaza maji na kichimba bwawa kubwa la Mifugo.

    Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA,Mhandisi Clement Kivegalo akizungumza na waandishi wakati wa kutembelea kijiji Cha Msomera kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika eneo hilo,amesema hadi kufikia mwakani kijiji hicho kitakuwa cha mfano kupata maji safi na salama.

    Mhandisi Kivegalo amesema hadi sasa utekelezwaji miradi ya maji Msomera imefikia zaidi ya asilimia 80, ambapo visima vitatu virefu vimechimbwa na vinatoa Maji zaidi ya lita 775,000 na mahitaji yote ni lita 450,000.

    Amesema pia RUWASA inaendelea na mradi wa kuchimbwa bwawa ambalo litakuwa na Maji Lita milioni 725 ambazo zitatumiwa na Mifugo na binaadamu..

    Meneja RUWASA mkoa wa Tanga, Upendo Omary amesema katika mradi huo hadi sasa Bomba zenye urefu wa kilomita 14 tayari zimechimbiwa chini na lengo kusambaa kilomita 20.8.

    Amesema katika mradi huo tayari matanki yamendaliwa na baadhi yameanza kupokea maji kuna Tanki lita 10,000 na jingine Lita 167,000 na kutakuwa na vituo 24 vya kutoa Maji.

    Meneja wa RUWASA wilaya ya Handeni,Hosea Joseph amesema watu 17,000,watanufaika na mradi huo wakiwepo watu 6036 ambao ni wenyeji wa Kijiji hicho.

    Amesema Bwawa katika Kijiji hicho litakamilika May 2023 lakini pia kuna mradi wa kujenga maeneo ya mifugo kunywa maji ambayo yatakamilika karibuni.

     

    Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Msomera , Martin Ole Ikayo alipongeza Serikali na Rais Samia Suluhu kwa msaada mkubwa uliotolewa kwa Kijiji hicho.

    “Sisi tunapongeza sana Rais Samia Suluhukwa maendeleo makubwa katika Kijiji chetu na uamuzi kuletwa wananchi wa Ngorongoro Msomera leo tuna shule, Sekondari na msingi , Kituo cha afya ,tuna umeme na Maji”amesema.

    Ikayo amesema shida ya Maji katika Kijiji imekwisha na sasa maji yameanza kutoka na hadi nyumbani kwake na RUWASA imefanya kazi kubwa sana katika Kijiji hicho.

    Kijiji Cha Msomera kinaendelea kupokea wananchi ambao wanachama kwa hiari katika eneo la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.

    Mwisho
    .

    Post Views: 51
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam,
    Next Article VILIO VYATAWALA MTOTO ANAEDAIWA KUUAWA HIFADHINI! MAGAZETI YA LEO A24TV

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.