Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Break News»RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMWAPISHA IGP WAMBURA MKACHAPE KAZI

    RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMWAPISHA IGP WAMBURA MKACHAPE KAZI

    0
    By arushatv on July 20, 2022 Break News
    Na Mwandishi wa A24Tv .Dodoma

     

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvalisha Cheo kipya cha Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP) aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camillus Mwongoso Wambura kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi  katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwapisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camillus Mwongoso Wambura kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi (IGP) katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma 

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwapisha aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Nyakoro Sirro kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbawe katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma 

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwapisha Balozi Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Zambia katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma 

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwapisha Dkt. Suleiman Haji Suleiman kuwa Balozi katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma 

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi Camillus Mwongoso Wambura mara baada ya kumwapisha kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma 

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi Camillus Mwongoso Wambura na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Nyakoro Sirro mara baada ya kumwapisha (IGP) Wambura kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi Ikulu Chamwino Jijini Dodoma

     Balozi Dkt. Suleiman Haji Suleiman kushoto, Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule, Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Simon Nyakoro Sirro na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camillus Mwongoso Wambura wakila kiapo cha maadili ya Uongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa rasmi na Mhe. Rais Samia Ikulu Chamwino Jijini Dodoma 

     

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali katika Hafla ya kumwapisha Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Mwongoso Wambura na baadhi ya Mabalozi aliowateua kwenye Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na CP Mussa Ali Mussa kushoto, Kamishna wa Fedha na Lojistik CP Liberati  Sabas Materu, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi CP Awadhi Juma Haji, na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad katika Hafla ya kumwapisha (IGP) Camillus Mwongoso Wambura Ikulu Chamwino Jijini Dodoma 

    ……………………………….

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameunda Kamati na Sekretarieti zitakazoshauri namna ya kuleta mabadiliko ya utendaji kazi  wenye matokeo bora katika vyombo vya utendaji haki. 

     

    Rais Samia amesema hayo katika hafla ya uapisho wa Viongozi mbalimbali iliyofanyika Ikulu Chamwino, akieleza kuwa Kamati hiyo itaongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Mohamed Chande Othman. 

     

    Aidha, Rais Samia amesema Kamati hiyo itaanza kulifanyia kazi Jeshi la Polisi na baadae katika majeshi mengine ya ulinzi na vyombo vya utendaji haki.

     

    Rais Samia pia amesema Serikali itapitia na kurekebisha miundo, mifumo ya ajira na mafunzo, mifumo ya upandishaji vyeo, madaraka na taaluma za kijeshi. 

     

    Masuala mengine ni kutoa mafunzo kwa majeshi ya ulinzi kuhusu matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na mahusiano ya Jeshi la Polisi na Taasisi zingine ikiwemo Kanuni na Sheria zinazoongoza Taasisi hizo.

     

    Kwa upande mwingine, Rais Samia amelitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa ufanisi, na kuimarisha usalama wa raia na mali zao na kuzingatia haki za binadamu 

    Post Views: 108
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWATOTO WA NNE WALIO FARIKI DUNIA KWA KUNYWA SUMU VIPIMO VYAFIKA KWA MKEMIA MKUU
    Next Article WAREMBO 50 KUTEMBELEA VIVUTIO VYA TANZANIA VIKIWEMO VYA ROYAL TOUR

    Related Posts

    MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMETOA MILION 33 KUNUNUA UNGA WA LISHE KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

    February 9, 2023

    KOREA KUSINI NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA WALETA PIKI PIKI MPYA ZA KUTUMIIA UMEME

    February 5, 2023

    BREAKING NEWS : MUSA JUMA MWENYEKITI MPYA JOWUTA SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO

    January 29, 2023

    WAFANYA BIASHARA SAMUNGE JIJINI ARUSHA WAPOKEA MILLIONI 100 KUTOKA KWA NABII MKUU GEORDAVIE WAHIDI MAKUBWA KATIKA KUKUZA MITAJI YAO

    January 27, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.