Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»MILLIONI 500 KUTUMIKA UJENZI WA BARABARA MONDULI MJINI.

    MILLIONI 500 KUTUMIKA UJENZI WA BARABARA MONDULI MJINI.

    0
    By arushatv on July 10, 2022 Habari

    Na Mwandishi wa A24Tv Munduli .

    Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa amekagua ujenzi wa barabara za Monduli Mjini zinazojengwa kwa Kiwango cha Lami , Pamoja na soko kuu la Monduli.

    Fredrick Lowassa amesema Fedha zinazotumika katika ujenzi huo ni Fedha zilizotoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwenda kwa Wabunge ambapo yeye ameelekeza Fedha hizo kutumika katika ujenzi wa barabara ndani ya wilayani hiyo.

    Kwa Upande wake Eng Janeth Mkoreha Meneja Tarura -Monduli, amewahakikishia Wananchi wa eneo hilo kukamilika kwa Barabara hiyo kwa Wakati pamoja na Mitaro kufanyiwa kazi kwa wakati.

    Ukaguzi huo wa barabara umeenda sambamba na ukaguzi wa soko kuu la Monduli Mjini Ambapo Awali akizungumza Mwenyekiti wa soko hilo Josephat Mbilinyi ameomba soko hilo kukarabatiwa , pamoja na malalamiko ya kutopewa mikopo kama wajasiriamali kutoka Halmashauri ndipo Mbunge Kumuagiza Mwenyekiti huyo siku ya Jumanne kufika ofisini kwake kwa ajili ya kuchukua fedha shilingi Millioni tatu na laki Nane (3.8) kwa ajili ya ukarabati wa paa la soko hilo.

    Post Views: 55
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleYANGA YAWEKA HISTORIA YAMPATA RAIS MPYA ! MAGAZETI YA LEO NA A24TV
    Next Article VIGOGO WAZITO WA CCM KUTIMKIA NCCR MAGEUZI WATAKA URAIS 2025 MAGAZETI YA LEO A24TV

    Related Posts

    Maafisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini waaswa kutangaza mafanikio ya utekelezaji wa MKUMBI

    March 30, 2023

    SHIRIKA La Umeme Tanzania (TANESCO), limezindua Programu ya Mpango wa miaka minne wa jinsia

    March 30, 2023

    Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameridhishwa maendeleo ya miradi ya ujenzi inayosimamiwa na Ofisi hiyo

    March 30, 2023

    KILELE CHA TUZO YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU ,APRIL 13 2023 KUFANYIKA DAR

    March 30, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.