Site icon A24TV News

DIWANI MSOFE SISI ATUWEZI KUSHIKWA MASIKIO NINAUZOEFU TUNATAKA KIKAO RASMI

Na Mwandishi wa A24tv.

SAKATA la Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela kuwaonya  madiwani wa Jiji la Arusha kuacha kutumika limechukua sura mpya  baada ya madiwani kumjibu wakielezea kusikitishwa na hatua yake ya kuwasema mbele ya wataalam huku akiwaombea mabaya.

Wakiongea kwa nyakati tofauti diwani wa kata ya Daraja Mbili, Prosper Msofe na diwani wa Ngarenaro, Isaya Doita walisema kuwa wao ni madiwani kwa awamu ya tatu sasa hivyo wanajielewa na wanapoingia kwenye vikao wanakuwa wanabishana kwa hoja na si majungu kama ambavyo RC Mongela alisema.

Diwani wa kata ya Daraja Mbili, Msofe alisema kuwa lengo lao madiwani ambao ninwawakilishi wa wananchi ni kutaka kujua fedha zilizoletwa kwenye halamshauri ziko wapi, zimefanya nini na hayo madeni yanagodaiwa yanatokana na nini

 

“Jiji lina hali mbaya jiji lina uwizi mkubwa hivyo huwezi kuzungumzia maendeleo bila kushughulikia wezi wakaondoka.Pesa zilikuja leo tuna madeni tunataka kujua fedha zilikwenda wapi tunataka kujua hayo tu. Sina shida na meya tena ni rafiki na ndugi yangu,” alisema Msofe na kuongeza.

…Tunataka meya atuambie fedha zilizoletwa halmashauri zilikwenda wapi na kwa nini tuna madeni leo,”.

Aidha diwani huyo alikanusha madai ya kuwa wanatumiwa na  mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo ingawa alimwagia sifa akidai kuwa ni mbunge mahiri na makini anayejua wajibu wake huku akidai kuwa mara nyingi mtu akiwa makini watu hawampendi.

Msofe alisema kuwa aliyekuwa mkurugenzi wa jiji la Arusha, Dk John Pima ambaye kwa sasa yupo mahabusu kwenye gereza la kisongo akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi hakuwahi kuitenga fedha za maendeleo kwa ajili ya kata la daraja mbili huku akimshukuru mbunge, Gambo kwa kumpatia shilingi 50 milioni kwa ajili

“Sijui masuala ya mgao unaodaiwa kuombwa na madiwani hayo mambo ya mgao waulizwe mkurugenzi Pima meya na vijana wao madiwani watatu walikuwa nao pamoja,”

Hata hivyo alimpongeza Kaimu Mkurugenzi wa jiji, Hargeney Chitukuro kwa kile alichoeleza  kuwa ameweza kufika kwenye kata yake na amekuwa akimpa ushirikiano wa hali juu katika kuwahudumia wananchi huku akimuombea awezw kuthibitishwa kushika nafasi hiyo.

“Mkurugenzi huyu kateuliwa kukaimu tu tunamng’oaje? Kikubwa tu waitishe vikao vinavyopaswa kuitishwa wasikilize kero. Njia ya kumaliza matatizo ni mazungumzo na si kutisha twendeni kwenye vikao halali tujadili matatizo ya jiji la Arusha wananchi wanasubiri maendeleo tuweze kusonga mbele na chama chetu kishinde kwa kura nyingi uchaguzi ujao,” alisema Msofe na kuongeza.

…Kimsingi wizi wowote kwenye jiji ni lazima kamati ya fedha iiutambue lakini hiyo inategemea  kama ni kamati inayojifahamu. Kwa sababu kila mwezi kamati inakaa kuangalia mapato yaliyokusanywa matumizi yaliyofanyika na matumizi yanayokwenda kutumika kulingana na bajeti yote ya halmashauri,”.

“Sasa endapo kamati hii inakaa kila mwezi halafu hawajui kilichokusanywa, hawajui kilichotumiwa, hawajui fedha zimeenda wapi sasa hiyo ni kamati  gani?” na kuongeza

…Ni jambo rahisi sana manake mwisho wa yote ni lazima tujue, ni lazima baraza la madiwani liambiwe kamati ya fedha ilifanya haya,  ili wajirekebishe lakini kukaa kimya bila kujadili kujua tatizo lilikuwa wapi basi litajirudia tena zitaibiwa nyingine tena,”.

Kwa upande wake diwani wa Ngarenaro, Doita alisema kuwa amesikitishwa mno na kauli za RC za kuwatuhumu madiwani kwa ujumla wao kwa mambo ambayo hayajui jambo alilshauri kama wapo madiwani wenye matendo hayo wakatajwa kwa majina.

” Madiwani hatuaminiki tunakuwa watu wa majungu, fitina na chuki. Akatuambia tutakaa hapa (Arusha) hatutaenda mahali popote mpaka tupauke. Mimi kama Dita diwani wa kata ya Ngarenaro jambo hilo lilinishangaza sana,” alisema Doita na kuongeza

 

…Sikujua mkuu wa mkoa alikuwa na hasira gani kwa sababu yeye ni mlezi na kiongozi wetu wa mkoa hivyo kama kulikuwa na tofauti yoyote angeweza kutuita madiwani wote tukaonana naye akatueleza kuwa tunaenda isivyo lakini si kuja kutushambulia mbele ya wataalam na kumwambia mkurugenzi hawa watu ishi nao kwa akili hawaaminiki ni kwamba anatengeneza ufa kati yetu na watendaji,”.

Doita alisema kuwa wao kama madiwani wanaaminika kwa wananchi waliowachagua na chama chao CCM hivyo akadai hajui majungu anayosema ni yapi.

Alisema ni vema kama kuna madiwani wamepotoka RC akawataja kwa majina lakini si kuwahukumu kwa ujumla wao kuwa ni wachafu na hawafai kuwa viongozi jambo alilodai kuwa limemsikitisha, limemuumiza na limemkatisha tamaa sana yeye binafsi.

“Yeye ni kiongozi wetu aliteuliwa na mheshimiwa Rais na sisi tulichaguliwa na wananchi ni vema tukakaa pamoja tuweze kupatana kusema tunashikiliwa akili na mtu mmoja si kweli mimi nina akili zangu na Gambo ana za kwake,” alisema Doita na kuongeza

..Tunakutana pale halamshauri kila mmoja wetu kwa ajili ya kuleta maendeleo lakini kusema tunamfuata mtu mmoja. Sisi si mazuzu kiasi hicho kweli tumedhalilika lakini hakuna cha kufanya. Kama tumemkosea tunamuomba radhi lakini nadhani jambo kubwa hapa tumekosea wapi, tumemkosea nani katika lipi, majungu ni yapi na fitina ni zipi,”.

“Kwa nini anamtahadharisha Mkurugenzi wetu atuogope sisi tutaenda naye kwenye vikao tutafanyaje maamuzi na mtu anayetuogopa, wakuu wa idara hata wananchi waliotuchagua watatuaminije. ,”.

“Tumemkwaza RC kwenye nini, wezi kukamatwa ni chukizo kwetu? Si ni furaha waliotuibia wamekamatwa. Wewe ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama watu wamekamatwa wameiba fedha za halamshauri mkondo wa sheria unaendelea wewe unawapiga madiwani,”.

Doita alisema kuwa RC alisema madiwani watapauka sana lakini yeye atajitahidi kuoga na maji mengi ili asipauke.

” Tulishtuka sana sijui kosa langu ni nini ningependa kujua kama kuna mahali popote nimewahi kumfanyia majungu mkuu wangu wa mkoa nimuombe msamaha lakini kunijumuisha kuwa nimefanya majungu imeniuma kwa sababu mimi niko wazi tu , Ngarenaro wananijua,” alisisiza Doita.