Site icon A24TV News

WAGOMBEA WA UWT TUFUATE TARATIBU ZA UCHAGUZ ! GAUDENSIA KABAKA MWENYEKITI WA UTW. TAIFA

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa amewataka wanawake wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Jumuiya hiyo kuwaheshimu viongozi wao walioko mada dearakani na kuwataka pamoja na kuheshimu kanuni za uchaguzi.

Kabaka amesema hayo Jijini Arusha wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ambapo alipata fursa ya kufanya mkutano na wanawake wa UWT mkoa wa Arusha uliofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Arusha.

“Uchaguzi ni Demokrasia na kila mwanachama ana haki ya kuvhagua na kuchaguliwa lakini niwatake wanawake wote wenye nia ya kugombea waje kwa utaratibu,wawaheshimu viongozi wao walioko madarakani kwa kipindi hiki na kufuata kanuni na taratibu za uongozi”.

Amesema wanawake wa Umoja huo kufanya kazi kwa kushirikiana na kupendana na kuachana na tabia za kupanga safu kwa sababu hazina tija na badala yake washirikiane na viongozi walioko madarakani kwa kuwa kazi ya kiongozi ninkuonyesha njia.

“Tambueni kuwa kila kiongozi atapimwa kwa kazi yake kwa sababu mwisho wa siku watapimwa kulingana na kazi walizozifanya kwa kipindi chao cha uongozi wa miaka mitano hivyo hakuna sababu ya kupanga safu . Wanawake wenzangu naomba sana tuheshimiane na kupendana na huo ndiyo msingi wa maendeleo”.

Alisema uhai wa Jumuiya Gaudensia aliwataka viongozi kuhamasisha wanachama kulipa ada kwa sababu tamwimu zinaonyesha kwamba kat ya wanachama wa Jumuiya hiyo 60,000 wanachama 48,000 siyo kutokana na kutolipa ada za uanachama kwa wakati.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Stephan aliwataka wana CCM mkoani humo kuendelea kupendana kudumisha mshikamo badala ya kutafutiana figisu ndogondogo ambazo hazina afya kwa CCM .

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Yasimin Bachu alisema maagizo yote yaliyotolewa na mwenyekiti huyo wa Taifa watayafanyia kazi na kwamba changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa ni mashine za usajili kwa ajili ya kusajili wanachama kwa mfumo wa kielektroniki 

Mwisho