Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»SABAYA NA WENZAKE SABA WASHINDA KESI YA PILI WACHIWA HURU

    SABAYA NA WENZAKE SABA WASHINDA KESI YA PILI WACHIWA HURU

    0
    By arushatv on June 10, 2022 Habari
    Na Geofrey Stephen Arusha

    Arusha.Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri kugubikwa na utata, hivyo kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yanawakabili na kuwatia hatiani

    Wakili mauna akizungumza na vyombo vya habari nje ya mahakama

    Mbali na Sabaya wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya

    .Hata hivyo Sabaya, Nyegu, Aweyo na Msuya wataendelea kubaki mahabusu katika gereza la Karanga kwa kuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi

    Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Juni 10 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo.

    Hii ni kesi ya pili Sabaya kushinda ambapo Mei 6, 2022 na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, walishinda rufaa iliyokuwa ikisikilizwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, waliyokata kupinga hukumu ya miaka 30 iliyokuwa imetolewa na na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

    Hakimu Kisinda amesema kuwa mbali na sababu hizo, mahakama imegundua kuwa hati ya mashitaka ilikuwa na mapungufu na kuwa ushahidi uliotolewa dhidi yao mahakamani hapo haujaweza kuthibitisha mashtaka hayo.

    Post Views: 112
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleKESI YA MAKONDA YAPIGWA CHINI! ALIFUNGUA KUBENEA MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV
    Next Article UTATA MZITO WAIBUKA MGOGORO LOLIONDO MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.