Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Break News»RAIS SAMIA AMTEUA MKUU MPYA WA MAJESHI NCHINI

    RAIS SAMIA AMTEUA MKUU MPYA WA MAJESHI NCHINI

    0
    By arushatv on June 29, 2022 Break News
    Na Mwandishi wa A24Tv .
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali na amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (Chief of Defence Forces – CDF).
    Kabla ya Uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi (Chief of Operations and Training).
    Rais Samia pia amempandisha Cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali na amemteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff – C of S).
    Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini (Commissioner for Research and Military Development) katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
    Vile vile amemteua Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
    Uapisho utafanyika tarehe 30/06/2022 saa saba mchana Ikulu, jijini Dar es Salaam.

     

    Post Views: 95
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleAWESO BODI ZA WAKURUGENZI WA MAJI NCHINI FUATILIENI MIRADI YA MAJI KWA UKARIBU
    Next Article YANGA YAWEKA HISTORIA! CDF MPYA HUYU HAPA MAGAZETI YA LEO A24TV

    Related Posts

    MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMETOA MILION 33 KUNUNUA UNGA WA LISHE KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

    February 9, 2023

    KOREA KUSINI NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA WALETA PIKI PIKI MPYA ZA KUTUMIIA UMEME

    February 5, 2023

    BREAKING NEWS : MUSA JUMA MWENYEKITI MPYA JOWUTA SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO

    January 29, 2023

    WAFANYA BIASHARA SAMUNGE JIJINI ARUSHA WAPOKEA MILLIONI 100 KUTOKA KWA NABII MKUU GEORDAVIE WAHIDI MAKUBWA KATIKA KUKUZA MITAJI YAO

    January 27, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.