Site icon A24TV News

Majangili Sugu yakamatwa na Meno ya Tembo Matano Lushoto

Na Geofrey Stephen lushoto

Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majangili sugu wamekatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro baada ya kukamatwa na meno ya tembo matano yenye uzito wa kilo 24 yenye tahamani ya mamilioni ya pesa wakisafirisha na usafiri aina ya pikipiki.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro,Kamishina Msaidizi wa Polisi,Saimoni Maigwa ilieleza kuwa majangili hayo yakiwa katika usafiri wa pikipiki mbili aina ya King Lion yakifunga kwa ustadi mkubwa nyara hizo za serikali katika mfuko wa salfeti walikamatwa juni 20 mwaka huu majira ya saa 7.30 mchana katika kijiji cha Malolo wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

Taarifa iliwataja waliokamatwa ni pamoja na mzee mwenye umri wa miaka 73 aliyetambuliwa kwa jina la Hassan Shauri mkulima mkazi wa kijiji cha Manolo,Eliud Gadi{32} dereva mkazi wa Kijiji Manolo na mtuhumiwa wa tatu Godson Elikunda{27} dereva na Mkazi wa Manolo.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo ilieleza kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni kufuatia operesheni iliyofanywa na askari wa ofisi ya Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa wa Kilimanjaro[RCO] kwa kushirikiana na askari wa Shirika Hifadhi za Taifa{TANAPA}.

Taarifa ya Kamanda ilieleza kuwa pikipiki mbili zilikamatwa katika tukio hilo ikiwemo moja yenye namba za usajili Mc 459 BWQ aina ya king Lion ilikuwa ikiendeshwa na mtuhumiwa Godson Elikuda na nyingine yenye namba za usajili mc 152CCQ aina ya King Lion iliyokuwa ikiendeshwa na Eliud Gadi.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kamanda huyo ilieleza kuwa Gadi akiwa amembeba Hassan Shauri ambaye ndio inadaiwa kuwa ndio mwenye meno hayo ya tembo.

Taarifa iliendelea kueleza kuwa chanzo cha kukamatwa kwa meno hayo ni kutaka kuyauza na kujipatia kipato isivyo halali wakati wakijua wazi kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na meno hayo ya tembo yalikuwa yamefungwa katika mfuko wa salfeti na kufungwa katika kiti cha pikipiki.

Kamanda katika taarifa yake alieleza kuwa thamani ya meno hayo tembo haijajulikana na watuhumiwa wote bado wanashikiliwa na jeshi la polisi na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili.

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Kalist Lazaro amewataka wakazi wa wilaya Lushoto kuacha mara moja kujishughulisha na biashara ya ujangili kwani vyombo vya ulinzi na usalama katika Mikoa ya Tanga na Kilimanjaro viko macho na vitawasaka wote wenye kufanya biashara hiyo haramu.

Lazaro alisema wakati wa kufanya ujangili katika wilaya yake imepitwa na wakati kwani unaipaka matope wilaya hiyo bila sababu za msingi na wale wote wenye ni ya kufanya biashara hiyo hawataachwa salama kwani dola itawakamata na kuwafikisha katika vyombo vya kimahakama.

’Nataka wakazi wote wa Wilaya ya Lushoto kufanya biashara halali yenye kujiingizia kipato na wale wenye kufanya biashara haramu kwa kutaka utajili wa haraka hawataachwa salama’’ alisema Lazaro

 

Mwisho