Site icon A24TV News

CORRDO SPRING HOTEL YAMALIZA DENI LA BILIONI 13 SASA HIKO MIKONO SALAMA !

Na Joseph Ngilisho ARUSHA

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya mjini Kati ,Arusha,limewashukuru na kuwapongeza waumini wake kwa kuinusuru hoteli ya kitalii ya nyota tatu ya Corridor Springs ambayo ni Mali ya kanisa Hilo isiuzwa kutokana na deni kubwa la mkopo lililofikia kiasi Cha sh,bilioni 13.5.

Akiwashukuru waumini wa kanisa Hilo waliofurika Katika ibada maalumu ya shukrani iliyofanyika katika kanisa Hilo usharika wa Kimandulu jijini hapa ,Askofu Mkuu Solomon Massangwa alisema waumini wa kanisa hilo wameliheshimisha kanisa kwa kukubali kuchangia na hatimaye kumaliza Deni Hilo.

Alisema ilifika mahala walitofautiana na baadhi ya viongozi wenzake huku wengine wakiwa tayari kuuzwa kwa hoteli hiyo iliyozinduliwa na rais was awamu ya tano Jakaya Mrisho Kikwete desemba 11,2008.

“Nawashukuru Sana waumini waliosimama imarabkupigania hotel yetu isiuzwa na leo tunamshukuru Mungu kwa miujiza hii tumemaliza Deni lililokuwa tishio na kama Mungu hakusimama na sisi kututetea Leo hii ingekuwa aibu”alisema Askofu Massangwa.

Akisoma taarifa ya deni hilo Mwenyekiti wa bodi wa hotel hiyo, Godwin Kimaro alisema Mwaka 2007 Dayosisi iliingia makubaliano na benki ya CRDB na kuchukua mkopo wa sh,bilioni 4.26 pamoja na kurithi Deni la sh,bilioni 2.2 ambalo kanisa ilikopa kutoka Sacco’s ya Makanisa iitwayo Oikocredit kiasi kilichofikia jumla ya sh, bilioni 6.48.

Alisema kuchukuliwa kwa mkopo huo 2007 Hadi 2011 marejesho ya mkopo huo hayakufanyika na hivyo kulimbikiza riba na mkopo na kufikia kiasi Cha sh, bilioni 8.73.

Alisema April Mwaka 2015 uongozi wa Dayosisi chini ya askofu Solomon Massangwa walifanya kikao na benki namna ya kurekebisha Deni Hilo ambalo lilifikia kiasi Cha sh, bilioni 11.4 pamoja na riba ya benki zaidi ya bilioni 2.

“Katika mazungumzo hayo Benki ilikubali kulipwa kila mwezi sh,milioni 68,639,701 kwa muda wa miaka 9 Hadi 2024.

 

Alisema Dayosisi ilifanya mikakati mbalimbali ya kupata Fedha ikiwemo michango ya waumini wote ambayo imefanikisha kumaliza Deni hiyo kabla ya wakati wa makubaliano,hatua ambayo kanisa limefanya ibada yakumshukuru Mungu.

Akiongelea hali ya hotel hiyo alisema mapato yamepanda kutoka milioni 459 mwaka 2015 Hadi kufikia sh,bilioni 1.259 Mwaka 2021 ambalo ni sawa na ongezeko la asilimia 274.

Aihuo

alisema wageni wa hotel wameongezeka kutoka 5912 mwaka 2015 mpaka 21,694 mwaka 2021 sawa nanongezeko la asilimia 367.

Awali mwasisi wa hotel hiyo askofu wa Dayosisi ya Tabora, Isaac Kisiri akiwashukuru waumini hao kwa umoja wao na kuwezesha kulipwa kwa Deni Hilo ambapo Deni Hilo liliwekwa kwenye kundi la wadaiwa sugu na kuwataka kuendeleza umoja huo

Ends…

.