Site icon A24TV News

AWESO BODI ZA WAKURUGENZI WA MAJI NCHINI FUATILIENI MIRADI YA MAJI KWA UKARIBU

Na Geofrey Stephen Arusha.
Waziri wa maji Juma Aweso amezitaka bodi za wakurugenzi wa Maji hapa nchini kuhakikisha  wanafanya juhudi kubwa za kuzipatia jamii za kitanzania maji karibu na mahali wanapoishi ili kuweza ili kuweza kutimiza adhima kuu ya serekali kutoa huduma ya maji kwa asilimia 95 hapa nchini.

Rai hiyo ameitoa leo hii Jijini Arusha wakati waziri wa maji  akifungua Mafunzo ya Siku Tatu ya kujengea uwezo wajumbe wa bodi na Menejiment  za Mamlaka  maji safi na Usafi wa mazingira zipatazo 25 yaliyofanyika jijini hapa ambapo lengo kuu lilikuwa kuwapa ujuzi juu ya usimamizi wa Mamlaka zao za Maji kama wajumbe wa Bodi.

Amesema kuwa mafunzo haya ya siku tatu ni matumaini kuwa yata wajengea uwezo Wajumbe hao na kuwataka kuhakikisha wajumbe hao wa bodi wanafanya usimamizi wa pamoja na kuchukua maamuzi makali katika mamlaka hizo.

Naye katibu mkuu wizara ya Maji enginia Antoni Sanga amewataka Wajumbe wa bodi kukaa na watumishi wa Idara za maji ili kuweza kuzielewa vizuri na kuweza kuzijua changamoto walizo nazo na kuweza kuzitatua sambamba na kufahamu kazi zinazofanywa na mamlaka zetu tunazozisimamia sisi bodi ya Wakurugenzi.

Pamoja na Bodi kutakiwa kuchukua hatua stahiki katika uongozi wa mamlaka ikiwemo maswala ya kinidhamu wahakikishe yanatatuliwa mapema na kuwambia kuwa  sasa hivi wizara ya maji sio ya kulalamikiwa bali ni  kutatua changamoto za maji.

Akizungumza kwa niaba ya Wenyeviti wa Bodi za maji Mwenyekiti wa Bodi ya maji ya Mamlaka ya maji safi na Maji taka jijini Arusha Dokta Richard Masika amesema amemuhakikisha kuwa kutokana na mafunzo haya ya siku tatu wana uhakika wa kwenda kuzisimamia mamlaka hizi vizuriwaa uweledi.

Mwisho .