Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Mahakamani»ALIYEKUA MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA PIMA NA WENZAKE WASOMEWA MASHTAKA MAPYA 6

    ALIYEKUA MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA PIMA NA WENZAKE WASOMEWA MASHTAKA MAPYA 6

    0
    By arushatv on June 21, 2022 Mahakamani

    Na Mwandishinwa A24Tv Arusha 

    Aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima (44) na wenzake wawili leo Juni 22, 2022 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakikabiliwa na kesi nyingine ya uhujumu uchumi yenye mashtaka sita ikiwemo mawili ya utakatishaji fedha.

    Wengine ni Mariam Mshana (40), aliyekuwa mkuu wa idara ya fedha ya halmashauri hiyo na Innocent Maduhu (40) aliyekuwa mkuu wa idara ya mipango ya uchumi.

    Mbali na watuhumiwa hao, wengine ni Nuru Ginana na Alex Daniel ambao walikuwa wachumi katika jiji hilo, nao walifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kukamilisha dhamana ambapo kupitia mawakili wao waliieleza mahakama hiyo kuwa hawajakamilisha masharti ya dhamana.

    • Katika a kesi hiyo Jamhuri inawakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Janeth Sekule, Wakili wa Serikali, Charles Kagilwa na Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Richard Jacopiyo huku washtakiwa hao wakiwakilishwa na Mawakili Valentino Nyalu na Sabato Ngogo.

    Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 5/2022, washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa sita ambapo kosa la kwanza linalowakabili ni ufujaji na ubadhirifu wa Sh103 milioni, kosa la pili na la tatu ni kutumia nyaraka kwa malengo ya kumdanganya mwajiri.

    Kosa la tano linalomkabili Maduhu ni utakatishaji fedha huku la sita likiwa utakatishaji ambalo linawakabili wote watatu.

    Wote walikana kutenda makosa hayo ambapo upande wa Jamhuri ulieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na hakimu

    Mwakisu aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 5, 2022.

    Post Views: 113
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleDPP AKATA RUFAA KESI YA SABAYA MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV
    Next Article THIBITINI UBORA BADALA YA KUDHIBITI BUNIFU – PROF MDOE

    Related Posts

    Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetoa amri ya kufika mahakamani kwa wajibu maombi kwenye kesi ya kulazimishwa kupotea

    March 23, 2023

    MFANYA BIASHARA WA MADINI YA TANZANITE SAITOTI NA WENZAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI WASOMEWA MASHTAKA YANAYO WAKABILI

    March 17, 2023

    RUFAA YA WANANCHI WA LOLIONDO YASIKILIZWA NA JOPO ZITO LA MAJAJI WATANO

    February 7, 2023

    JELA MIAKA MINNE KWA KUMKATA BOSI WAKE KIGANJA CHAMKONO

    January 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.